SERIKALI imekiri kuwa haijalipa fidia kwa
wananchi wa Wilaya ya Arumeru ambao walitakiwa kupisha upanuzi wa miradi ya
EPZ.
Kauli
hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Teu
na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na zoezi la upimaji wa uthamini
kutokukamilika.
Teu
alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA)
aliyetaka kujua ni lini serikali italipa fidia kwa mashamba ya wananchi wa
Malula, Kata ya King’oli baada ya mashamba yao kuingizwa katika mipango ya EPZ.
Akiendelea
kujibu swali hilo, Teu alisema Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Mamlaka ya
EPZ ilibainisha eneo lenye ukubwa wa ekari 4,000 chini ya Kijiji cha Malula.
Alisema
juhudi za kutwaa eneo hilo mwaka 2008 zilianza ambapo EPZ ilituma sh milioni 22
kwenda Halmashauri ya Meru kwa ajili ya uhamasishaji, upimaji na uthamini wa
eneo zima.
Naibu
huyo alisema kati ya miaka ya 2009 hadi 2011, uongozi wa Wilaya ya Arumeru kwa
kushirikiana na Mamlaka ya EPZ ulifanya vikao mbalimbali vya upimaji na
uthamini wa eneo husika pamoja na makubaliano ya wamiliki.
Hata
hivyo, alisema wananchi hao wanaruhusiwa kuendelea na kazi za kilimo cha mazao
ya muda mfupi katika maeneo hayo.
0 comments:
Post a Comment