UCL-FAINALI: BAYERN MUNICH MABINGWA ULAYA!
>>BAO LA DAKIKA YA 89 LA ROBBEN NI
MUUAJI!!
BAO LA DAKIKA YA 89
la Arjen Robben limefuta gundu kwake na Bayern Munich katika Fainali za UCL,
UEFA CHAMPIONZ LIGI, baada ya Bao hilo kuipa ushindi wa Bao 2-1 Bayern dhidi ya
wenzao wa Germany Borussia Dortmund katika Mechi iliyochezwa Wembley Stadium
Jijini London Jumamosi Usiku.
Bayern walipoteza Fainali mbili za UCL katika
Miaka mitatu iliyopita, ikiwemo kutolewa kwa Mikwaju ya Penati na Chelsea Mwaka
jana tena katika Uwanja wao wenyewe Allianz Arena, lakini safari hii waliibuka
Washindi wa Kombe hili kwa mara ya 5.
Ni Real Madrid, mara 9, na AC Milan, mara 7, ndio
wameshinda Kombe hili mara nyingi kupita Bayern Munich.
Kwa Kocha wao, Jupp Heynckes, huu ni ushindi
mtamu kwa vile anastaafu na nafasi yake kuchukuliwa na aliekuwa Kocha wa
Barcelona, Pep Guardiola kwa ajili ya Msimu ujao.
MAGOLI:
Bayern Munich 2
-Mandzukic Dakika ya 60
-Robben 89
>>BAO LA DAKIKA YA 89 LA ROBBEN NI
MUUAJI!!
Borussia Dortmund 1
-Mandzukic Dakika ya 68
[Penati]
Mara baada ya Filimbi ya mwisho kulia, Arjen
Robben alitokwa machozi kwani alikuwepo wakati Bayern Munich inapoteza Fainali
mbili kwa Inter Milan, Mwaka 2010, na Chelsea, 2012, ambapo alikosa Penati
katika Mikwaju ya Penati iliyoipa Chelsea Ubingwa, na vile vile akiwa na Chelsea
katika Miaka ya 2005 na 2007 walitolewa kwenye Nusu Fainali ya Mashindano haya
na mara zote hizo walikuwa ni Liverpool ndio waliowabwaga.
Mechi hii ilitangaza vyema Soka la Kushambulia la
Germany.
VIKOSI:
BAYERN MUNICH: Neuer; Lahm,
Boateng, Dante, Alaba; Martinez, Schweinsteiger; Robben, Muller, Ribery;
Mandzukic.
Akiba: Starke, Van Buyten,
Shaqiri, Luiz Gustavo, Tymoshchuk, Pizarro Gomez
BORUSSIA DORTMUND: Weidenfeller;
Pisczcek, Subotic, Hummels, Schmelzer; Bender, Gundogan; Blaszczykowski, Reus,
Grosskreutz; Lewandowski.
Akiba: Langerak, Kirch, Santana,
Kehl, Leitner, Sahin, Schieber.
REFA: Nicola Rizzoli [Italy]
UCL-MABINGWA WALIOPITA:
MSIMU
|
BINGWA
|
1955–56 | Real Madrid |
1956–57 | Real Madrid |
1957–58 | Real Madrid |
1958–59 | Real Madrid |
1959–60 | Real Madrid |
1960–61 | Benfica |
1961–62 | Benfica |
1962–63 | Milan |
1963–64 | Internazionale |
1964–65 | Internazionale |
1965–66 | Real Madrid |
1966–67 | Celtic |
1967–68 | Manchester United |
1968–69 | Milan |
1969–70 | Feyenoord |
1970–71 | Ajax |
1971–72 | Ajax |
1972–73 | Ajax |
1973–74 | Bayern Munich |
1974–75 | Bayern Munich |
1975–76 | Bayern Munich |
1976–77 | Liverpool |
1977–78 | Liverpool |
1978–79 | Nottingham Forest |
1979–80 | Nottingham Forest |
1980–81 | Liverpool |
1981–82 | Aston Villa |
1982–83 | Hamburg |
1983–84 | Liverpool |
1984–85 | Juventus |
1985–86 | Steaua BucureÈ™ti |
1986–87 | Porto |
1987–88 | PSV Eindhoven |
1988–89 | Milan |
1989–90 | Milan |
1990–91 | Red Star Belgrade |
1991–92 | Barcelona |
1992–93 | Marseille |
1993–94 | Milan |
1994–95 | Ajax |
1995–96 | Juventus |
1996–97 | Borussia Dortmund |
1997–98 | Real Madrid |
1998–99 | Manchester United |
1999–2000 | Real Madrid |
2000–01 | Bayern Munich |
2001–02 | Real Madrid |
2002–03 | Milan |
2003–04 | Porto |
2004–05 | Liverpool |
2005–06 | Barcelona |
2006–07 | Milan |
2007–08 | Manchester United |
2008–09 | Barcelona |
2009–10 | Internazionale |
2010–11 | Barcelona |
2011–12 | Chelsea |
0 comments:
Post a Comment