USAJILI WA TANZANIA AMRI KIEMBA ASAINI YANGA, NIYONZIMA ASAIN MIAKA MIWILI
KAMPUNI
ya S. S. Bakhressa ilipoanzisha timu ya soka ya Azam FC, viongozi na
mashabiki wa klabu kongwe za Simba na Yanga walidhani ni nguvu ya soka.
S.
S. Bakhressa ikapiga hatua ya pili kwa kujenga uwanja wa kisasa,
Chamazi, Temeke, Dar es Salaam, ikiwa ni ishara ya dhamira ya kufanya
mapinduzi ya soka nchini.
Mbali
ya kujenga uwanja wa mazoezi (unatumika hata kwa mashindano) na uwanja
mkubwa wa kisasa ambao ujenzi wake ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete
hivi karibuni, S.S. Bakhressa imeingia hatua nyingine kubwa kwa
kuanzisha kituo cha televisheni cha Azam TV.
Moja
ya malengo ya Azam TV inayojenga barabara ya Nyerere ni kutumia kiasi
cha Sh. 1.5 bilioni kuonyesha moja kwa moja mechi za Ligi Kuu ya
Tanzania Bara.
Ikiwa
itapata haki ya kuonyesha ‘live’ mashindano hayo, taarifa zinasema Azam
TV imejipanga kutoa Sh. 100 milioni kwa kila timu kati ya 14
zitakazoshiriki msimu ujao wa ligi hiyo. Hii ni neema kubwa kwa klabu
zote hasa changa.
Hii
ina maana sasa angalau kila timu, itaweza kujikimu kwa kiasi chake na
kuweka karibu uwiano sawa wa kuchuana na timu zenye uwezo mkubwa wa
kifedha kama Simba, Yanga na Azam FC iliyo chini ya kampuni ya S. S.
Bakhressa.
Kwa
hiyo, timu zisizo na wadhamini mkubwa na ambazo ndiyo kwanza zimepanda
daraja kama Ashanti United ya Ilala, Mbeya City ya Mbeya na Rhino ya
Tabora na hata zilizopo kama Coastal Union zitanufaika kwa kiasi kikubwa
na ujio wa udhamini wa Azam TV.
Timu
zilizoshuka daraja za Toto African, African Lyon na Polisi Morogoro
zitakuwa zinasikitika neema kuja kwenye ligi wakati zimetupwa nje.
Msimu
uliopita tuliiona Toto ya Mwanza ikishiriki kwa tabu ligi hiyo huku
wachezaji wake wakilala katika basi wakati mwingine huku chakula pia
kikiwa shida. Hali hii inachangia kwa kiasi kikubwa timu hizi ambazo
hazipo chini ya taasisi kubwa kufanya vibaya hasa katika mechi zake za
umbali mrefu na wakati mwingine hata zile za katika kituo chake.
Kwa vyovyote vile Azam TV inakuja kuleta ushindani mkubwa siyo katika udhamini tu, bali hata urushaji wa vipindi vya michezo.
Lakini
Simba na Yanga zilizoanzishwa kabla ya uhuru ‘zinapanga’ hujuma. Simba
wanadai kiasi cha Sh. 100 milioni ni kidogo na hakilingani na hadhi yao
na pia hawawezi kulipwa sawa na timu nyingine za ligi hiyo.Mwenyekiti
wa Simba, Ismail Rage amenukuliwa na gazeti moja la michezo akisema
anakubaliana na wazo la Azam TV, lakini kiasi hicho cha fedha ni kidogo
kwao na hata siku moja timu haziwezi kulipwa haki sawa ya matangazo huku
akitolea mfano katika Ligi Kuu ya England.
Kwa
upande wa Yanga, Ofisa Habari wake, Baraka Kizuguto amesema hawezi
kuzungumzia vitu vya tetesi kwani Azam TV hadi sasa hawajawapelekea
taarifa rasmi kuhusu lengo hilo la kuonyeshwa kwa mechi zao msimu ujao.
“Sipo
katika nafasi nzuri ya kuzungumzia jambo hilo, kwani hatujataarifiwa
jambo lolote juu ya mpango huo wa Azam TV, wakituletea maombi yao, sisi
kama timu tutakaa na kutoa uamuzi,” anasema Kizuguto.
Hii
ina maana kwamba, kama Simba na Yanga zitabaki na mawazo hayo, Azam TV
inaweza kukwamishwa katika mpango huu na kubaki na ule wa kuonyesha
mechi za timu yao tu, kwani lengo lao ni kutangaza biashara zao.
Utaratibu
ni kwamba muda ukifika, uongozi wa Azam TV utaomba kibali cha kudhamini
Ligi Kuu kutoka Kamati ya Ligi ambayo itapanga kiwango baada ya kuteta
na klabu.
Vituo
vya TV vikionyesha ‘live’ mechi yoyote ya ligi hupaswa kulipa gharama
kufidia kiasi cha watu ambao hawataingia uwanjani na kutumia fursa hiyo
kurusha matangazo ya biashara. Azam TV haitazungumza na klabu binafsi.
Lakini
kwa desturi za Simba na Yanga, ambazo miaka nenda rudi ni kupanga
mikakati ya kuangushana, hata hili zinaweza kukwamisha. Kwa husuda
zitaweka mgomo ili mpango huu ufe ili zenyewe zibaki kutawala soka, timu
ndogo zibaki zikinyanyasika kama ilivyokuwa kwa Toto African
iliyopigana hadi inashuka daraja.
Rai
yangu kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kamati ya Ligi ni
kwamba, Simba na Yanga zisiachwe kuharibu mapinduzi ya soka yanayoletwa
na Azam TV.
HABARI HII IMETOLEWA KATIKA GAZETI LA MAWIO, IMEANDIKWA NA ELIUS KAMBILI
0 comments:
Post a Comment