Tuesday, 31 March 2015

MABEKI WAIPA USHINDI URENO, RONALDO KIMYA, GERMANY YASHINDA!


EURO2016Portugal wamekwea kilele cha Kundi I la EURO 2016 baada ya kuichapa Serbia 2-1:hapo Jana.
Bao za Portugal zilifungwa kila Kipindi na Mabeki wao Ricardo Carvalho na Fabio Coentrao huku mashine yao ya Magolj Cristiano Ronaldo akiwa kimya.
Bao la Serbia lilifungwa na Kiungo wa Chelsea Nemanja Matic.
Huu ni ushindi wa 3 mfululizo wa Portugal kwenye EURO 2016 chini ya Kocha mpya Fernando Santos ambae alishika hatamu mara baada ya kufungwa Mechi ya ufunguzi ya Kundi I na Albania.
Sasa Portugal wanaongoza Kundi I wakiwa Pointi 2 mbele ya Denmark wenye Mechi 1 mkononi.
Katika Kundi D, Germany wamerudi kwenye reli baada ya kuipiga Georgia Ugenini Bao 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Kwanza za Marco Reus na Thomas Muller.
Katika Mechi nyingine ya Kundi D, Scotland, wakicheza kwao huko Hampden Park Jijini Glasgow, wameicharaza Timu mpya Gibraltar Bao 6-1 lakini Wageni hao wameweka historia ya kufunga Bao lao la kwanza katika Mashindano ya UEFA tangu wajiunge nao.
   
EURO 2016
Jumapili Machi 29
MATOKEO
Romania 1 Faroe Islands 0
Scotland 6 Gibraltar 1
Northern Island 1 Finland 1
Albania 2 Armenia 1
Georgia 0 Germany 2
Hungary 0 Greece 0
Ireland 1 Poland 1
Portugal 2 Serbia 1
Jumanne Machi 31
2145 Israel v Belgium

0 comments: