Mashabiki na wapenzi wa klabu ya
Dar es Salaam Young Africans, ambao ndio wawakirishi pekee wa Tanzania
katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Africa, leo asubuhi
wameondoka nchini na kuelekea Zimbabwe kuishangilia timu yao
itakapominyana na FC Platinum wiki hii.
Mashabiki hao wameondoka kwa
usafiri wa basi dogo aina ya Toyota Coaster wakipanga kupitia Iringa,
Mbeya na Tunduma kasha kutumbukia Zimbabwe.
FC Platinum ambao ndio wenyeji wa
mchezo huo wa marudiano ambao utapigwa siku ya Jumamosi wiki hii,
watawakaribisha Yanga wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 5-1 kunako
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa kwanza.
Kikosi cha kazi cha Yanga, kitaondoka nchini kesho Jumatano kwa Usafiri wa ndege ya kukodi ya Serikali.
0 comments:
Post a Comment