KEPTENI wa Liverpool Steven Gerrard
ameomba radhi kwa kutandikwa Kadi Nyekundu Sekunde 38 tu baada ya kuingia
Uwanjani kwenye Mechi iliyochezwa Anfield na Timu yake kutandikwa 2-1 na
Manchester United hapo Jumapili.
Gerrard, mwenye Miaka 34 na ambae
anahamia huko Marekani kuchezea LA Galaxy mwishoni mwa Msimu, alitolewa nje na
Refa Martin Atkinson kwa kumkanyaga kusudi Ander Herrera wa Man United na sasa
atakosa Mechi 3 za Liverpool.
Akiongea mara baada ya Mechi hiyo,
Gerrard alisema: “Inabidi nikubali, uamuzi ulikuwa sahihi. Nimewaangusha
Wachezaji wenzangu na Mashabiki. Nawajibika kwa yote. Hata sijui nini kilitokea
labda kukumbwa na Herrera. Sisemi zaidi. Ila nimekuja hapa kuomba radhi.”
Wakati akipewa Kadi Nyekundu,
Liverpool ilikuwa nyuma kwa Bao 1-0 na hii pengine ni Mechi yake ya mwisho
dhidi ya Mahasimu Man United akiwa amevaa Jezi ya Liverpool Klabu ambayo
alianza kuichezea tangu 1998 na kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2005 pamoja na
Vikombe vingine 9.
Mechi ambazo atazikosa Gerrard akiwa
kwenye Kifungo chake cha Mechi 3 ni ile ya huko Ewood Park dhidi ya Blackburn
Rovers ya Marudiano ya Robo Fainali ya FA CUP, Mechi ya Ligi Kuu England huko
Emirates na Arsenal na ile ya Anfield na Newcastle hizi zikiwa Mechi kati ya 8
walizobakisha za Ligi.
0 comments:
Post a Comment