Polisi
nchini India wamemtia mbaroni mwanamume mmoja kuhusiana na ubakaji wa
mtawa mmoja wa Kanisa Katoliki katika makaazi ya watawa Magharibi mwa
Bengal.
Viongozi wa Kikristo nchini India wamekosoa Serikali kwa kuzembea katika kazi yake ya kukabiliana na uhalifu.Mshukiwa huyo alitiwa mbaroni mnamo Jumatano Usiku mjini Mumbai.
Amesafirishwa hadi Kolkata ili kufanyiwa mahojiano zaidi.
Yeye ni mtu wa kwanza kutiwa mbaroni kuhusiana na ubakaji huo uliofanyika katika makaazi ya watawa katika Ranaghat majuma mawili yaliyopita.
Washukiwa sita walioshiriki wizi huo wa ubakaji walinaswa katika kamera za CCTV. Kufuatia malalamiko kuwa Serikali hailichukulii swala hilo na umuhimu unaostahili Serikali sasa imekabili kesi hiyo kwa idara ya upelelezi.
Waziri Mkuu Narendra Mondi ameeleza masikitiko yake kuhusiana na shambulio hilo na kutoa zawadi kwa ye yote atakayesaidia kuwatia mbaroni walioshiriki katika uhalifu huo.
0 comments:
Post a Comment