Thursday, 26 March 2015

EURO 2016: MITANANGE KUENDELEA IJUMAA, COSTA, ROBBEN, RVP NJE!


EURO2016Vita ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, huko Ufaransa Mwakani, inaendelea kunzia Ijumaa hadi Jumanne kwa Mechi za Makundi ambayo yatafikia idadi ya Nusu ya Mechi zake zote.
Mechi 26 zinatarajiwa kuchezwa Wikiendi hii na kumalizika Jumanne kwa Mechi moja ambayo ni kiporo baada ya kuahirishwa hapo awali.
Spain, ambao ni Mabingwa Watetezi, watakuwa kwao Mjini Sevilla kucheza na Ukraine huku wote wakiwa wamefungana katika Nafasi ya Pili ya Kundi C wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Slovakia ambao watacheza na Timu ubwete Luxembourg.
Ijumaa, Spain watacheza Mechi yao bila ya Straika wao kutoka Chelsea, Diego Costa, ambae ni Majeruhi, na badala yake Kocha Vicente del Bosque amewaita Mastraika Chipukizi Alvaro Morata na Juanmi.
Siku hiyo hiyo Ijumaa, Harry Kane huenda akacheza Mechi yake ya kwanza kwa England ambao wanacheza na Lithuania Uwanjani Wembley, London wakitaka kuendeleza rekodi yao ya kushinda Mechi zao zote za Kundi E ambalo wanaongoza wakiwa na Pointi 12 zikiwa Pointi 6 zaidi ya Timu zinazowafuatia Slovenia, Switzerland na Lithuania.
Kane, Straika wa Tottenham mwenye Miaka 21, ameifungia Timu yake Bao 29 tangu mwanzoni mwa Msimu ikiwa pamoja na Hetitriki Wikiendi iliyopita walipoichapa Leicester 4-3.
Hiyo hiyo Ijumaa zipo Mechi zingine 3 za Kundi G ambapo Vinara Austria watasafiri kwenda kucheza na Liechtenstein, Sweden watakuwa Ugenini kucheza na Moldova na Russia wako Ugenini huko Monenegro.
Jumamosi, Vinara wa Kundi H Croatia, wanaofungana Pointi na Italy wote wakiwa na 10, watacheza na Norway wakati Itaky wako Ugenini na Bulgaria.
Kocha wa Italy, Antonio Conte, anatarajiwa kuwatumia Wachezaji wapya Watatu ambao ni Mzaliwa wa Brazil anaechezea Sampdoria, Eder, na Mzaliwa wa Argentina anaecheza Palermo, Franco Vazquez pamoja na Kiungo Mirko Valdifiori ambae ana nafasi kubwa kucheza kwa vile Mkongwe wa Juventus Andrea Pirlo ni Majeruhi na Daniele De Rossi hakuitwa.
Kundi A ambalo wamo Netherlands waliofungwa Mechi 2 kati ya 4 za kwanza, watacheza na Turkey Mjini Amsterdam bila ya Mastaa wao Majeruhi Arjen Robben na Robin van Persie wakati Vinara wa Kundi hili, Czech Republic watakuwa Nyumbani kucheza na Latvia, na Iceland, ambao wako Nafasi ya Pili, wako Ugenini huko Kazakhstan.
Israel na Wales, ambao hawajafungwa na wanaoongoza Kundi B, watakutana huko Haifi, wakati Belgium ambao pia wako Kundi hili wako Nyumbani kucheza na Cyprus wakati Bosnia-Herzegovina wako Ugenini kucheza na Andorra wakisaka ushindi wao wa kwanza.
Jumapili, Mabingwa wa Dunia Germany wanasafiri kwenda Tbilisi kucheza na Georgia katika Mechi ya Kundi D ili kufufua Kampeni yao ambayo iko mrama huku Vinara Poland wakiwa Dublin kucheza na Ireland ambao pamoja na Germany na Scotland wapo Pointi 3 nyuma ya Poland.
Scotland wapo kwao Glasgow kucheza na Gibraltar ambayo haipewi nafasi yeyote.
Jumapili hiyo hiyo, Vinara wa Kundi F ambao hawajapoteza Mechi, Romania, wapo kwao kucheza na Faroe Islands wakati Timu ya Pili Northern Ireland watacheza Nyumbani na Finland na Hungary pia wapo Nyumbani kuivaa Greece.
Katika Kundi I, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, anaweza kuipaisha Nchi yake Portugal kutwaa uongozi wa Kundi wakicheza kwao na Serbia kwa vile Denmark hawachezi.
EURO 2016
Ratiba
**Saa za Bongo
Ijumaa Machi 27
KUNDI C
2345 FYR Macedonia v Belarus
KUNDI C
2345 Slovakia v Luxembourg
KUNDI C
2345 Spain v Ukraine       
KUNDI E
2345 England v Lithuania
KUNDI E
2345 Slovenia v San Marino
KUNDI E
2345 Switzerland v Estonia
KUNDI G
2345 Liechtenstein v Austria
KUNDI G
2345 Moldova v Sweden
KUNDI G
2345 Montenegro vRussia
Jumamosi Machi 28
KUNDI A
1900 Kazakhstan v Iceland
KUNDI A
2100 Czech Republic v Latvia
KUNDI B
2100 Israel v Wales
KUNDI H
2100 Azerbaijan v Malta
KUNDI H
2100 Croatia v Norway
KUNDI H
2345 Bulgaria v Italy
KUNDI A
2345 Netherlands v Turkey
KUNDI B
2345 Andorra         v Bosnia and Herzegovina
KUNDI B
2345 Belgium v Cyprus
Jumapili Machi 29
KUNDI D
2000 Georgia v Germany
KUNDI D
2000 Scotland v Gibraltar
KUNDI F
2000 Northern Ireland v Finland
KUNDI F
2000 Romania v Faroe Islands
KUNDI I
2000 Albania v Armenia
KUNDI I
2245 Portugal v Serbia
KUNDI F
2245 Hungary v Greece
KUNDI D
2245 Republic of Ireland v Poland
Jumanne Machi 31
KUNDI B
2245 Israel v Belgium

0 comments: