Kiungo wa klabu ya Bayern Munich
Arjen Robben atakosekana uwanjani kwa muda wa wiki kadhaa baada ya
kuumia katika mechi iliyoisha kwa mabingwa hao wa bundesliga
kupokea kichapo cha 2-0 kutoka kwa Borrusia Monchenglabach licha ya
kucheza katika uwanjani nyumbani Allianz Arena, inasemekana kiungo huyo atakosa zaidi ya mechi 8
Mholanzi huyo alipata maumivu
hayo katika dakika ya 24 ya mchezo baada ya kuchezewa vibaya na beki
Tony Jantske na hivyo kutolewa nje akiwa amebebwa kwenye machela.
Hii ni habari mbaya kwa Arjen
Robben ambaye amerudi mazoezini hivi karibuni baada ya kuumia katika
mechi ya klabu bingwa dhidi ya Shaktar Donetsk Machi 12.
Kocha wa klabu hiyo mhispania Pep
Guardiola anakibarua kizito kuziba pengo la winga huyo machachari
ambaye anauwezekano mkubwa wa kukosa mechi za robo fainali za klabu
bingwa Ulaya dhidi ya FC Porto mwezi ujao.
Aidha Robben,31, atakosa mechi ya
timu ya taifa ya uholanzi dhidi ya Uturuki ambayo ni mechi ya kutafuta
tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa Ulaya mwaka 2016 na ile ya kirafiki
dhidi ya Hispania.
0 comments:
Post a Comment