Misri,
Ethiopia na Sudan zimetia saini mkataba wa kwanza kuhusu ugavi wa maji
katika ya Nile unaopitia mataifa hayo yote matatu.
Mkataba huo unafuatia ujenzi unaoendelea wa bwawa kubwa la ''the Grand Rennissance'' linalojengwa na Ethiopia katika mto Nile.Ujenzi huo umezua mzozo mkali wa kidiplomasia kati ya Misri na Ethiopia.
Mwandishi wa BBC nchini Ethiopia Emmanuel Igunza na maelezo zaidi.
Viongozi wa mataifa hayo matatu,walikutana jijini Khartoum Sudan kwa sherehe ya kutia saini mkataba huo ambao umetajwa kama hatua ya kwanza katika kutatua mzozo huo.
Bwawa hilo linalotarajiwa kugharimu takriban dola bilioni nne, litakamilishwa mwaka wa 2017 na kuwa moja ya mabwawa kubwa zaidi barani Afrika.
Ethiopia inasema itaisaidia katika kuzalisha nguvu za umeme kwa ajili ya viwanda vyake na pia inatarajia kuuza kawi kwa mataifa jirani.
Lakini akizungumza hii leo, Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi amesema mkataba huo unashiria nia ya mataifa yote kuleta maelewano kuhusu utumizi wa maji ya mto Nile.
Abdel Fattah Al Sisi alisema “Mradi huu wa bwawa la renaissance linashiria chanzo cha maendeleo kwa mamilioni ya raia wa Ethiopia kwa kuzalisha kawi safi,
lakini kwa ndugu zao wanaoishi katika kingo za mto huohuo wa Nile nchini Misri, na mabo idadi yao ni sawa, inashiria chanzo cha wasiwasi.
Hii ni kwa sababu Nile ndio chanzo chao ha peke cha maji, na hasaa chanzo cha maisha.”
Mara kwa mara Misri imepinga mradi huo ikisema huenda bwawa la Rennaissance likapunguza viwango vya maji kwa raia wake.
Hata hivyo Rais wa Sudan Omar al Bashir ametaka mataifa yote matatu kuhakikiha yanazingatia maendeleo lakini pia kutilia maanani maslahi ya nchi zote.
“Tunamini kuwa ushirikiano ndio njia ya pekee ya kuafikia maelewano na utangamano kati ya watu wetu, na kwamba bila ushirikiano, tutapoteza nafasi ya kuwa na masiha bora.
Kwa hivyo tunahitaji kufanya kazi pamoja kujenga mazingira ya ushirikiano na kukariri kwa maslahi ya kitaifa hayageuki na kuwa vikwazo kwa maslahi za kikanda na ujirani mwema.” Alisema rais Bashir
Ethiopia ilianza kubadilisha mkondo wa mto Nile mwezi Mei mwaka wa 2013, ili kujenga bwawa hilo linalotarajiwa kuzalisha megawati 6,000 za umeme litakapokamilika.
Misri kwa upande wake inaamini kuwa ina haki za kihistoria za mto huo kufuatia mikataba ya mwaka 1929 na 1959, inayoipa asilimia 87 ya maji ya mto huo, na pia uwezo wa kupinga miradi yoyote inayojengwa katika mto Nile.
0 comments:
Post a Comment