VENGU |
Taarifa za kufariki dunia kwa
Joseph Shamba maarufu kama Vengu, zimekanushwa vikali.
Kuanzia saa 4 asubuhi kumekuwa
na taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba Vengu wa kundi la Orijono Komedi amefariki
Dunia.
Vengu ameugua kwa takribani
miaka mitatu sasa hali yake ikiwa si nzuri.
Meneja wa kundi hilo, Seki David
amesema si kweli kuhusiana na taarifa hizo.
“Ni habari zisizo sahihi, Vengu bado ni mgonjwa na ningependa kuwaomba wanaosambaza taarifa hizo kutofanya hivyo,” alisema Seki.
0 comments:
Post a Comment