BAADA ya machungu ya kutandikwa 2-1
kwao Anfield na Mahasimu wao Man United Jumapili na pia Kepteni wao Steven
Gerrard kupewa Kadi Nyekundu katika Mechi hiyo hiyo na sasa kufungiwa Mechi 3,
balaa kwa Liverpool bado halijaisha kwani sasa FA imemfungulia Mashitaka
Sentahafu wao Martin Skrtel kwa kumkanyaga Kipa wa Man United David De Gea
katika Mechi hiyo hiyo.
Kwa vile tukio hilo la Skrtel,
ambalo lilitokea Dakika za Maheruhi halikuonwa na Refa Martin Atkinson, Kanuni
za FA, Chama cha Soka England, zinataka Jopo Huru la Marefa Watatu wa zamani
walipitie na ikiwa wote Watatu wataafiki linastahili Kadi Nyekundu basi
Mchezaji husika hufunguliwa Mashitaka.
Hayo ndio yaliyomkuta Skrtel,
Mchezaji wa Kimataifa wa Slovakia mwenye Miaka 30, ambae amepewa hadi Leo Saa 3
Usiku kujibu Shitaka lake.
Ikiwa atapatikana na hatia,
Sentahafu huyo atafungiwa Mechi 3 na atazikosa Mechi 2 za Ligi Kuu England za Aprili
4 huko Emirates na Arsenal na ile ya Anfield na Newcastle hapo Aprili 14 na
Marudiano ya FA CUP ya Robo Fainali huko Ewood Park na Blackburn Rovers hapo
Aprili 8.
Hizo pia ndizo Mechi ambazo Kepteni
Steven Gerrard atazikosa baada ya Kadi Nyekundu kwenye Mechi hiyo hiyo
aliyolambwa Sekunde 38 tu tangu aingie Uwanjani kutoka Benchi kwa kumkanyaga
kwa kusudi Ander Herrera wa Man United.
0 comments:
Post a Comment