Carlos Tevez Leo amefunga Bao 1 na la ushindi na kuipaisha Juventusbkuwa Pointi 17 juu kileleni mwa Serie A walipoifunga Genoa 1-0 ndani ya Juventus Arena Jijini Turin huko Italy.
Hilo ni Goli la Tevez la 24 Msimu huu na Juzi alipiga Bao 2 walipoichapa Borussia Dortmund huko Signal Iduna Park Bao 3-0 na kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mechi hii na Genoa Tevez, mwenye Miaka 31, alikosa Penati Kipindi cha Pili lakini Juve, wakicheza bila Kiungo wao mahiri Paul Pogba ambae ni majeruhi na atakuwa nje kwa Miezi Miwili, walilinda vyema Bao lao moja.
Sasa Juve wapo nijani kutwaa Taji lao la 20 la Ubingwa wa Italy na hili litakuwa ni la 4 mfululizo.
0 comments:
Post a Comment