Tuesday, 31 March 2015

STERLING AIZUNGUSHA ANFIELD KUSAINI MKATABA MPYA,


raheem-sterling2 0Raheem Sterling amelaumiwa na Veterani wa Liverpool Jason McAteer kwa kuzungusha kukubali Mkataba mpya na Liverpool.
Huku kukiwa na habari nzito kuwa Chipukizi huyo moto mwenye Miaka 20 anaechezea pia England yuko mbioni kwenda Spain kujiunga na Barcelona au Real Madrid, Liverpool iltaka haraka kumfunga kwa kumpa Mkataba mpya mnono lakini kambi ya Sterling imegoma.
Mkataba wa sasa wa Sterling na Liverpool unakwisha 2017.
Jason McAteer, Beki wa zamani alieichezea Liverpool Miaka mingi, anahisi Mchezaji huyo anashauriwa vibaya baada ya mazungumzo ya pande mbili kuvunjika na kupelekwa hadi mwishoni mwa Msimu kuanza upya.
McAteer amesema: "Mazungumzo yamekwama. Inaelekea Sterling anatafuta jambo! Lakini ajue hapa ni sehemu nzuri kubaki kwa Miaka kadhaa ili kukuza Soka lake badala ya kuhamia nje kwenye Utamaduni mwingine ambao unaweza kumwathiri!"

0 comments: