Timu
ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo imegawana pointi na timu ya
Malawi baada ya sare ya bao 1-1 kwenye mchezo ambao umepigwa kunako
Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Bao la Stars limefungwa na Mbwana Samatta akisawazisha bao baada ya kupokea pasi safi ya Ngassa kunako dakika ya 76.
Malawi walipata bao katika dakika
ya 4 kupitia kwa Esau Kanyenda kufatia mpira wa Kona baada ya Kipa
Mwadini Ally akapangu mpra na kuangukia miguuni mwa mchezaji wa Malawi
ambaye hakufanya makosa .
Katika kipindi cha pili ambapo
Tanzania ilionyesha kushambulia sana lango la Malawi, Cannavaro alikosa
bao katika dakika ya 52 baada ya kupiga kichwa safi laki ikawa sio
bahati kwa Tanzania.
Samatta alikosa bao dakika ya 57 baada ya kuwapiga chenga mabeki wa Malawi na kupiga shuti ambalo linatoka nje kidogo ya lango.
Dakika ya 60 Ngassa aliingia kuchua nafasi ya Chanongo .
Malawi ilimtoa John Banda na nafasi yake ikachukuliwa na kaka yake Frank Banda dakika ya 64.
Dakika ya 68 Amri Kiemba alitoka na nafasi yake ikachukuliwa na Salum Abubaka Sure Boy.
Ngassa alipiga shuti kalilakini linakuwa halina macho, ikiwa ni katika dakika ya 74.
John Bocco aliingia kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu katika dakika ya 80.
0 comments:
Post a Comment