Matokeo ya awali ya kura zilizopigwa siku ya jumamosi huko Nigeria zinaonesha kuwa kiongozi wa upinzani Muhammadu Buhari
anaongoza kwa zaidi ya kura milioni mbili zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambaye ni rais Goodluck Jonathan.Generali Buhari wa chama cha All Progressives Congress (APC) anaonekana kusajili matokeo mema mapema hata kabla ya kuhesabiwa kwa kura za mjini Lagos.
Matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria yanatarajiwa kutangazwa saa chache zinazokuja wakati majimbo yaliyosalia yakisubiriwa kutangaza matokeo yao.
Huku zaidi ya nusu ya matokeo yakiwa yametangazwa mgombea wa upinzani Muhammadu Buhari yuko mbele ya rais wa sasa Goodluck Jonathan.
Hata hivyo matokeo bado hayawezi kutabiriwa kwa kuwa majimbo yenye watu wengi kama Lagos na Rivers hayajatangaza matokeo yake.
0 comments:
Post a Comment