Imeamuliwa kuwa Fainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey, itachezwa Nou Camp, Nyumbani kwa Barcelona, hapo Mei 30 kati ya Athletic Bilbao na Barcelona.
Kawaida Fainali ya Kombe hili huchezwa Uwanja usio wa Timu iliyo Fainali lakini baada ya Real Madrid kugomea kutoa Uwanja wao Santiago Bernabeu ukaanza mvutano wa wapi Fainali hiyo ichezwe.
Kwenye Mkutano wa Shirikisho la Soka la Spain na Klabu hizo mbili, Kura ilitumika na Viwanja vya Sevilla, Vicente Calderon, na Mestalla wa Valencia kubwagwa na kuacha Viwanja vya Barca Nou Camp na San Mames cha Bilbao kwenye kinyang'anyiro.
Hatimae Nou Camp ilipita na hii itakuwa mara ya kwanza kwa Timu iliyo Fainali kucheza Fainali Uwanja wake wa Nyumbani tangu 2002 wakati Deportivo La Coruna walipoifunga Real Madrid Nyumbani kwao Santiago Bernabeu.
Mara ya mwisho kwa Nou Camp kuwa Mwenyeji wa Fainali za Copa del Rey ni 2010.
Ikiwa Barca watatwaa Kombe hili, ambalo wao wanaongoza kwa kulibeba mara nyingi, hii itakuwa mara yao ya 27 wakati Athletic Bilbao wakifuata kwa wingi wa kulitwaa kwa kulichukua mara 23.
0 comments:
Post a Comment