Mechi ya kufuzu ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Ulaya kati ya
urusi na Montenegro ilisitishwa baada ya wachezaji kutoka timu zote
kupigana uwanjani.
Awali mechi hiyo ilikuwa imesitishwa kwa dakika
30 baada ya mlinda lango wa Urusi kugongwa na kifaa na kisha kupelekwa
hospitalini.Wakati Urusi ilipopoteza penalti katika cha kipindi cha pili wachezaji na maafisa kutoka pande zote walianza kupigana.
Kisha mchezaji mwingine wa Urusi aligongwa wakati vifaa zaidi viliporushwa uwanjani hatua iliyomfanya refa kusimamisha mechi hiyo.
Hakuna timu iliyokuwa imefunga bao wakati huo na haijulikani hatua ambayo itachukuliwa na shirikisho la soka barani ulaya.
0 comments:
Post a Comment