Mcheza
tennis wa Marekani Venus Williams anaelekea kupambana na mdogo wake
Serena Williams katika fainali za Miami Open baada ya jana kumshinda
Caroline Wozniacki katika hatua ya 16 bora.
Awali mchezaji huyo hakuwa katika ubora wake kwa takribani miezi saba baada ya kugundulika kuwa hali yake ya kiafya kuwa si njema mnamo mwaka 2011, lakini sasa ameshinda michezo saba kati ya nane aliyocheza dhidi ya wachezaji walio katika viwango vya kumi bora. Wakati dada akifanya hayo Serena alimgaragaza Svetlana Kuznetsova kwa ushindi wa set 6-2 6-3 kuingia katika robo fainali.
0 comments:
Post a Comment