Mshambuliaji wa klabu ya
Liverpool na timu ya taifa ya England Daniel Sturridge ametolewa katika kikosi
cha timu ya taifa baada ya kufanyiwa uchunguzi hapo jana na kugundulika
anamaumivu makali juu ya paja.
Mchezaji huyo aliwasili jana
katika uwanja wa St.George Park ambapo kikosi hicho cha Roy Hodson kinafanyia
mazoezi ili kuonana na madaktari wa timu hiyo ambao baada ya kumfanyia
uchunguzi waliona majeraha hayo ambayo aliyapata katika mechi ya juzi
waliyofungwa na Manchester United.
Sturridge,25, amekuwa
mchezaji wa pili wa Liverpool kutolewa katika kikosi hicho baada ya hapo awali
Adam Lallama kutolewa kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja na
nafasi yake kuchukuliwa na kiungo wa Tottenham Hotspurs Ryan Mason ambaye
hajawahi kuichezea England hata mechi moja.
Hivyo wachezaji hao watakosa
mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa Ulaya 2016 dhidi
Lithuania itakayopigwa ijumaa hii kwenye uwanja wa Wembley na ile ya kirafiki
dhidi ya Italia kule Turin jumanne ijayo.
Aidha hili ni pigo kwa kocha
wa Liverpool Brendan Rodgers ambaye alimkosa Daniel Sturridge kwa muda mrefu
mwanzoni mwa msimu huu kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha
aliyoyapata wakati akiwa na timu ya taifa.
Diego Costa wa Hispania
Mshambuliaji wa klabu ya
Chelsea na timu ya taifa ya Hispania Diego Costa ametolewa katika kikosi cha
timu ya taifa baada ya madaktari wa timu hiyo kumfanyia uchunguzi na kugundua
kuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Imeripotiwa kuwa mshambuliaji
huyo aliumia katika mechi ya juzi jumapili ambayo Chelsea iliibuka na ushindi
wa 3- 2 dhidi ya Hull City iliyopigwa katika uwanja wa KC.
Taarifa kutoka chama cha soka
cha Hispania SFA inasema ” Tumepokea taarifa kutoka kwa daktari wa timu kuwa
Costa anamaumivu ya nyama za paja hivyo hataweza kucheza na hivyo atarudishwa
katika klabu yake kwa matibabu zaidi “
Hivyo Mchezaji huyo wa zamani
wa Atletico Madrid atakosa mechi ya timu ya taifa ya Hispania dhidi ya Ukraine
ijumaa hii ambayo ni yakutafuta tiketi ya kucheza fainali za mataifa Ulaya 2016
na ile ya kirafiki dhidi ya uholanzi.
0 comments:
Post a Comment