Tabora. Mahakama Kuu Kanda ya Tabora leo inatarajia kusikiliza kesi ya ugaidi dhidi ya makada watano wa Chadema iliyotolewa uamuzi na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa Tabora kuwa haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo .
Mahakama hiyo inatarajia kutoa uamuzi dhidi ya hoja zilizowasilishwa na mawakili wa uapnde wa utetezi, Peter Kibatala pamoja na Profesa Abdallah Safari kuwa sheria zilikiukwa katika kuwasilishwa kwa kesi hiyo.
Washtakiwa ni Evodius Justunian, (30) mkazi wa Bukoba, Osca Kaijage mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Seif Magesa mkazi Nyasaka Mwanza, Rajabu Daniel mkazi wa Dodoma na walikuwa wakishtakiwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Igunga kabla ya Henry Kilewo kuunganishwa katika kesi hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu, wakili Kibatala alisema kuwa katika Mahakama Kuu watahakikisha wanashambulia mashtaka hayo kwa kufuata sheria ili kila kitu kisikilizwe upya.
Alisema kuwa mashtaka hayo hayana mashiko ya
kuitwa makosa ya kigaidi na kuongeza kuwa Mahakama Kuu wataiomba
iyaangalie kwa mara ya pili kwa umakini zaidi.
Habari Na Mustapha Kapalata,
Mwananchi gazati
Posted Jumatatu,Julai22 2013
Posted Jumatatu,Julai22 2013
0 comments:
Post a Comment