MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia kwa dhamana Ludovick Joseph
anayeshitakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema
Wilfred Lwakatare, baada ya kusota rumande kwa zaidi ya miezi minne.
Ludovick
aliachiwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana baada ya kutimiza
masharti ya dhamana yaliyotolewa Juni 10 mwaka huu.
Washitakiwa
hao waliofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 18 mwaka huu,
wanakabiliwa na shitaka la kutaka kumdhuru Mhariri wa gazeti la
Mwananchi, Dennis Msacky kwa kutumia sumu.
chanzo HabariLeo
Tuesday, 16 July 2013
HOME »
» ALIYE SHITAKIWA NA LWAKATARE BWANA LUDOVICK JOSEPH ACHIWA HURU KWA DHAMANA
0 comments:
Post a Comment