Mkurugenzi
wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Wilfred Lwakatare, ambaye amelazwa kwenye Taasisi ya Magonjwa ya Mifupa
(MOI), akisumbuliwa na maumivu ya shingo pamoja na mkono anaendelea
vizuri.
Ofisa
Habari wa Taasisi hiyo, Patrick Mvungi, aliiambia NIPASHE jana kuwa
Lwakatare ambaye alifikishwa Hostitalini hapo Jumanne ya wiki hii,
anaendelea na matibabu huku akiwa chini ya jopo la Madaktari ambao
walimfanyia vipimo alipofikishwa hospitalini hapo.
Mvungi
aliongeza kuwa Lwakatare alikuwa analalamikia maumivu ya shingo pamoja
na mkono, na jopo hilo la madaktari wanaangalia ni jinsi gani wataweza
kulishugulikia tatizo hilo ambalo anasema limekuwa likimsumbua kwa muda
mrefu kidogo.
0 comments:
Post a Comment