Bara la Asia lina soko kubwa sana la pembe za Ndovu
Pembe haramu za ndovu zilizokuwa zinasafirishwa kutoka Uganda hadi Malaysia, zimenaswa katika bandari ya Mombasa pwani ya Kenya.
Pembe hizo zilikuwa zimefunikwa kiasi cha kufanana na samaki waliokaushwa.
Mzigo huo wa takriban pembe 770 kutoka nchi Uganda, ulikuwa unapelekwa Malaysia.
Walanguzi hao pia walikuwa wamebeba samaki
waliokuwa na harufu mbaya ambayo huwachukiza Mbwa maalum wa uchunguzi,
kulingana na msemaji wa shirika la ulinzi wa wanyapori nchini Kenya Paul
Udoto.
Pembe za Ndovu zina soko kubwa sana barani Asia, ambazo hutumiwa kwa vitu vya urembo.
Serikali ya Kenya iliharamisha biashara za pembe
za ndovu mwaka 1989, huku viwango vya uwindaji haramu wa Ndovu
vikipungua pakubwa, lakini pameanza kuonekana ongezeko la uwindaji
haramu tena wa Ndovu katika miaka ya hivi karibuni.
Bwana Udoto alisema stakabadhi kuhusu pembe hizo zilolionyesha kuwa zilisafirishwa kutoka Uganda kwa gari tarehe 12 mwezi Juni.
Gari hilo kisha likaegeshwa katika kituo cha
mafuta mjini Mombasa, eneo la kufanyia biashara hadi mzigo huo
ulipofikishwa bandarini.
Thamani ya pembe hizo badi haijabainika kwa mujibu wa bwana Udoto.
0 comments:
Post a Comment