TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Serikali ya Mpito ya Madagascar, Mheshimiwa Andry Rajoelina amewasili nchini jana mchana kwa ziara ya kikazi katika Tanzania ambako baadaye atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar Es Salaam, Mheshimiwa Rajoelina amepokelewa na mwenyewe wake, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC-Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Asasi hiyo, Rais Kikwete ndiye amepewa jukumu na viongozi

wenzake wa nchi wanachama wa SADC kutafuta suluhisho la mgogoro wa kisiasa katika Kisiwa cha Madagascar.
Viongozi hao wawili watakutana Ikulu, Dar es Salaam baadaye leo kuzungumzia hali ya kisiasa nchini Madagascar ambako Rais Kikwete atamweleza Mheshimiwa Rajoelina kuhusu matokeo ya kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa Asasi (SADC-Troika-Summit) kilichofanyika chini ya uenyekiti wake juzi, Jumamosi usiku, mjini Pretoria, Afrika Kusini.
Naye Raojelina anatarajiwa kumwelezea Rais Kikwete kuhusu hali ilivyo katika Madagascar na hasa kuhusiana na jitihada za kuandaa Uchaguzi Mkuu nchini ambao umekuwa unakumbwa na changamoto kadhaa.
Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Julai, 2013
0 comments:
Post a Comment