Friday, 5 July 2013

BASI LA KWANZA LIENDALO KASI LATARAJIWA KUWA BARABARANI JULAI 2015 (DSM)

UONGOZI wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (DART), umesema basi la kwanza la kutoa huduma hiyo litaanza kusafirisha abiria Julai mwaka 2015. Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa DART, Asteria Mlambo, alisema hayo juzi mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa.

Alisema baada ya kukamilika kwa mradi huo na kuanza shughuli zake, utaondoa daladala zaidi ya 3,000 katikati ya Jiji. Alisema wamiliki wa daladala hizo, wanaombwa kuunda umoja wao, utakaotambuliwa rasmi ili kuwa na mabasi maalumu, yatakayotumika kwa usafiri huo wakiwa kama ni wabia.

Kaimu Mkurugenzi wa Usafirishaji na Maendeleo wa DART, Hassani Uledi alisema usafi huo pia utakuwa ni rafiki kwa watu wenye ulemavu wa viungo, ambao wanaweza kuingia ndani ya mabasi yaendayo haraka na baiskeli zao za magurudumu manne au matatu.

 

0 comments: