Friday, 19 July 2013

EPUKA KUTAPELIWA GARI KWA KUKODISHWA -KWA KISINGIZIO CHA MRADI WA GESI -MTWARA SOMA HAPA


Picture: Haika Laware, Mbezi Garden Hotel
Haika Lawere
JIHADHARI NA UTAPELI WA KUKODI MAGARI KWA INVESTORS GAS YA MTWARA!

Ndugu zangu wenye magari 4 wheels drive e.g. Landcruisers Vx/v8, prados, Vogue, X5, Murano, Audi, Santafee, Pajero etc na Mabasi, kuna makampuni hewa ya wazungu investors hewa yameingia Dar es Salaam wakisema wanahitaji aina hiyo ya magari iliyotajwa hapo juu, kwa ahadi ya kukulipa $100 hadi $200 kwa siku, kwa hiyo kwa mwezi unapata kitu km $3,000 hadi $6,000!

Ni kwamba, wakifanikiwa kupata magari kati ya 10 hadi 20, wanayachukua, wanayaendesha na madereva wao, wanayatorosha nje ya Tz kwenda Rwanda, Burundi, Zambia, Congo nk!

Watu wameshalizwa jamani kwa kuibiwa magari ya kifahari. Mimi wamenifuata watu wa namna hii kunipa hii deal, nikakataa! So guys be careful wit these sweet deals!


Angalizo hili limenukuliwa kutoka kwa Haika Lawere, Mkurugenzi wa Mbezi Garden Hotel

 

0 comments: