Mtuhumiwa Richard Mwangusi
Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limemkamata na kumtupa mahabusu mhubiri Richard Mwangusi, raia wa nchini uganda kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii baadhi ya watu wameeleza kusikitishwa na kito cha utapeli kinachofanywa na mhubiri huyo ambaye amekuwa akiishi katika nyumba ya kulala wageni ya Wihanzi mjini Iringa kuwa amekuwa akiwataka watu kutuma pesa kwa njia ya M-PESA kuanzia TSh 10,000 na kuendelea iwapo wanahitaji kupanga muda wa kuongea na mhubiri huyo kupitia simu ya kiganjani.
Baadhi ya wananchi ambao walitoa malalamiko yao leo walidai kuwa mhubiri huyo amekuwa akitumia namba ya simu ya Lodge ya Wihanzi ambayo ni 0262700222 kwa kuwataka watu wenye matatizo kupiga simu kwa namba hiyo na mara baada ya kupiga simu mhudumu ambaye yupo zamu amekuwa akimtaka mtu aliyepiga simu kueleza shida yake na mara baada ya kueleza iwapo anataka kuongea na mhubiri huyo amekuwa akitaka kutumiwa kwanza kiasi cha fedha kwa namba ya mhubiri huyo ndipo apewe huduma anayotaka.
Mmoja kati ya watu ambao wamepata kulizwa na mhubiri huyo amedokeza kuwa namba za mhubiri huyo amezipata kupitia kituo kimoja cha Radio mjini Iringa na kutokana na baadhi ya watu kutoa ushuhuda kuwa wamepona magonjwa sugu ndio sababu ya kuchukua namba yake ili kuweza kuombewa pia ila baada ya kuchukua namba hiyo amejikuta akiishia kuliwa pesa bila kupewa huduma husika.
Pia alisema kila anapomtafuta mhubiri huyo kwa njia ya simu ili kuombewa amekuwa akimtaka kuongeza pesa zaidi ili kuombewa hadi kupona jambo ambalo amekuwa akijiuliza kama kwa sasa injili ya biashara na kama biashara basi ni vyema wahubiri watangaze bei kamili ili mtu anunue kulingana na uwezo wake.

0 comments:
Post a Comment