Janeth
Jackson (32), mke wa mfanyabashara maarufu wa madini mkoani Arusha
anadaiwa kupanga njama za kumuua mumewe wa ndoa na mtoto wa mume huyo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas, amesema mwanamke huyo aliwaagiza watu wawili kumsaidia kutekeleza azma yake hiyo ya kumuangamiza mumewe, mtoto wake na ndugu wanaoweza kumzuia urithi.
Kamanda Sabas, amesema Julai 16 mwaka huu majira ya saa mbili usiku, jeshi la polisi lilipokea taarifa kutoka kwa mfanyabiashara huyo kuhusu kuwepo mpango ulioandaliwa na mke wa mfanyabiashara huyo wa kumuua yeye na mwanaye na ndugu wa mume waishio mkoani Kagera ili aweze kumiliki mali.
Amesema katika mpango huo ulioandaliwa na mke wa mfanyabiashara huyo alituma watu wawili kutoka jijini Arusha, eneo la Moshono kwenda mkoani Kagera ili kufanya mauaji hayo na kisha wangelirejea jijini Arusha ili kukamilisha mpango huo kwa kumuua mfanyabiashara huyo.
Amesema jeshi la polisi lilituma makachero wake na Julai 17 mkoani Kagera ili kufuatilia tuhuma hizo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Novatus Elias Mrisha, kabla ya kutekeleza mpango huo huku mwenzake akikimbia na wanaendelea kumsaka.
Kamanda Sabas amesema kuwa katika mohojiano na Mrisha, mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika katika mpango huo baada ya kutumwa na mke wa mfanyabiashara huyo
Jana, mwanamke huyo ambaye ni mkazi wa Moshono Jijini Arusha alipandishwa katika mahakama ya wilaya ya Arusha iliyopo Sekei, pamoja na mtuhumiwa Novatus Elias Mrisha, jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha/Arumeru, Devotha Kamuzora na kusomewa makosa mwili ya kula njama ya kutaka kumwua Simon Jackson Manjuru Kaijage.
Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Edna Kasala alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa wote wawili walitenda kosa la pili la kula njama na kutaka kumwua Desderi Sabas (12) ambaye ni mtoto wa nje wa mume huyo anayeishi Bukoba mkoani Kagera.

CHANZO WAVUTI.COM
0 comments:
Post a Comment