MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKIFUNGUA MKUTANO WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA(RCC) JIJINI MBEYA
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PHILIPO MULUGO AKICHANGIA JAMBO WAKATI WA KIKAO HICHO
MKUU WA WILAYA WA MBEYA DR. NORMAN SIGARA AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO HUO
MEYA WA JIJI MBEYA ATANAS KAPUNGA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
WAJUMBE WAKIWA WANAFUATILIA MKUTANO HUO
Songwe
ndilo jina lililopendekezwa kuitwa kwa Mkoa Mpya utakao gawanywa kutoka
Mkoa wa Mbeya ambao utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba
ambapo Makao makuu ya Mkoa huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.
Mkoa wa zamani Mkoa wa Mbeya utabaki na Wilaya za
Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu yatabaki pale pale Jijini Mbeya.
Kupatikana
kwa jina hilo na mwafaka huo umetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri
ya Mkoa uliofanyika jana katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa
na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.
Jina la Mkoa huo Mpya limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na
Mto mkubwa unaoitwa Songwe ambao umezipitia Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.
Hata
hivyo kuhalalishwa kwa jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Raisi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa
mapendekezo hayo ya RCC.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Baada ya kupatikana kwa mkoa mpya wa mbeya baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kupitia mtandao huu kwa jina lililochaguliwa ni zuri ila makao makuu yangekuwa wilaya ya mbozi ili iwe rahisi kwa wananchi wote na hasa wa wilaya ya Momba kupata huduma muhimu za kimkoa bila kusafiri umbali mrefu wa kwenda chunya. Bwana Wifred Ngajilo ambae yeye ni mkazi wa Mbozi amelalamika kuwa chunya itakuwa mabli kwenda toka mbozi.
Kazi kwenu wasomaji toa maoni yako.
0 comments:
Post a Comment