Monday, 22 July 2013

MAKAHABA WALALAMIKA WANAFUNZI WANAWAPOKONYA WATEJA

  Eldoret
Barabara moja katika mji wa Eldoret. Picha/MAKTABA 
Na TITUS OMINDE
 

MAKAHABA NCHINI KENYA mjini wa Eldoret wamelalamikia kuharibika kwa biashara mjini humo kutokana na ongezeko la wanafunzi ambao wamejiingiza katika biashara hiyo.
Wahudumu hao wa biashara ya ngono wanadai kuwa wanafunzi wamejingiza katika biashara hiyo ikiwa ni pamoja na wanafunzi wa shule za misingi.

Kwa mujibu wa makahaba hao miongoni mwa wanafunzi hao ni pamoja na watahiniwa wa kidato cha nne kutoka katika shule moja mjini humo.
“Kuna wasichana fulani kutoka vyuo vikuu ambao wameharibu biashara sana wengi wao huja kutafuta senti za anasa wakiwa chuoni, mbali na hao wa vyuo vikuu vile vile kuna wanafunzi wa shule za upili. Kwa mfano kuna wasichana wawili, mmoja wa kidato cha nne na mwingine cha tatu ambao huja hapa kutegea wateja,” alisema mmoja wa wahudumu hao.
Wahudumu hao walisema wateja wengi kwa sasa hupendelea wanafunzi haswa wa shule za upili ambao hulipisha hela kidogo.
Makahaba husika walisema wanafunzi wengi hujitosa katika biashara hiyo wakati wa likizo na msimu wa kuvuna ngano katika jimbo la Uasin Gishu.

Ngano

Mbali na biashara hiyo kunoga msimu wa kuvuna ngano mjini Eldoret wahudumu hao walifichua kuwa kuna soko jingine nzuri wakati wa msimu sawia na huo katika eneo la Narok.
“Yenyewe biashara huwa mzuri hapa msimu wa kuvuna ngano. Si hapa tu pekee kwani mwezi wa saba na wa nane biashara hiyo hunoga katika jimbo la Narok hapa hivi najiandaa kuhamia Narok,” alisema.

     Hata hivyo  kuna baadhi yao ambao wanataka wahisani kuwasiadia kwa kuwapa mtaji wa kuanzisha biashara mbadala ili kujitoa katika biashara hiyo ambayo ni haramu.
“Ningependa kama kuna wahisani waje wanisaidie nipate mtaji wa kuanzisha biashara nikipata pesa za kuanzisha biashara siwezi nikaendelea na hii biashara ngumu” alisema mmoja wao.


chanzo swahilihub .com

0 comments: