BONDIA wa ngumi za mateke ‘Kick boxing’, Japhet Kaseba, ameisihi
serikali kuwekeza kwenye mchezo huo na sekta hiyo kwa ujumla ili iweze
kutoa ajira kwa vijana wenye vipaji mbalimbali.
Kaseba anayeing’arisha Tanzania katika ndondi aina ya Kick Boxing,
alisema juzi kuwa kama serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni,
Vijana na Michezo, ingefanya uwekezaji kwenye sekta hiyo, ingetoa ajira
kwa vijana wengi.
“Tanzania imejaliwa kuwa na vijana wengi wenye vipaji, lakini vimekosa
sapoti ya serikali, tungekua na serikali inayojali na kuthamini michezo
kwa vitendo, sekta ya michezo ingekuwa msaada kwa vijana wengi,”
alisema.
Kaseba anatoa pia wito kwa mabondia chipukizi kuwa wavumilivu katika
kujifunza mchezo huo licha ya kuwepo kwa changamoto nyingi zinazoweza
kuwavunja moyo.
“Kinachotakiwa kufuatwa katika mchezo huu ni nidhamu, bondia akiwa na
nidhamu pamoja na kufuata sheria zote za mchezo huo atafanikiwa,”
alisema.
na Mwandishi wetu Tanzania dima
0 comments:
Post a Comment