Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ndiuka A Siwema Ally akisoma barua aliyoandikiwa mwanamke huyo na polisi Makambako |
SIKU moja baada ya mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Stella Mnyagani mwenyeji wa Mabadaga Chimala wilaya ya Mbarali mkoa wa Mbeya atelekeza mtoto wake wa kiume nje ya duka moja eneo la Ndiuka 'A' katika Manispaa ya Iringa.
Mengi yafichuka juu ya mwanamke huyo kutelekeza mtoto wake inasadikika mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi ya kuuza bar katika eneo hilo la Ndiuka na baadhi ya maeneo ya mji wa Iringa.
Mashuhuda waliobahatika kumwona mwanamke huyo wanadai kabla ya kutenda unyama huo wa kutupa mtoto mwanamke huyo alikutwa katika mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa likiwemo eneo la Ofisi za Tanesco akiwa amekaa kando ya barabara kabla ya kuondoka na kuelekea eneo la Ndiuka ambako aliamua kumtekeleza mtoto huyo .
Mtoto huyo wa kiume anayekadiliwa kuwa na mwaka mmoja alikutwa juzi majira ya saa 2 usiku katika eneo hilo la Ndiuka 'A' huku akiwa na vifurushi viwili vya nguo pamoja na dawa za aina mbali mbali .
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Ndiuka A Siwema Ally alisema kuwa mtoto huyo aliokotwa na wasamaria wema na kupelekwa kwake kabla ya kuchukuliwa na polisi na kupelekwa kituo cha yatima cha Daily Bread Life MInistries kinachomilikiwa na Neema Mpeli
Mwanamke huyo pia aliacha namba za simu ambazo ni 0766663281 inayomilikiwa na Kastori Mlyatage pamoja na namba ya Mahenge wa Mabadaga 0753493063 na namba ya mama Fatuma 0757 519270 pamoja na barua inayoonyesha alisaidia kituo cha polisi Makambako kwa ajili ya Kwenda Singida
CHANZO na GODWINFRANCES BLOB
0 comments:
Post a Comment