IDD AZAN |
Idd Azzan amekaririwa na HabariLeo (via) jana
akisema kuwa hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya
ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa
ujumla. Akasema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake amedhamiria
kumshushia heshima na huenda ana jambo limejificha.
Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.
Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.
Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwa nini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo?
Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani
katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.
Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernard na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.
Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu.
Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni.
Alipoulizwa
kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya
vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, Azzan alisema: “Ni ngumu kusema
hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema
kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya
uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za
kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua.”
Source: habarileo gazeti
0 comments:
Post a Comment