Mshambuliaji
wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar, ameshinda tuzo ya Mpira wa Dhahabu kama
mchezaji bora wa Kombe la Mabara, Confederations Cup.
Katika michezo mitano ya timu
yake kwenye Kombe la Dunia, Neymar, alifunga kwenye mechi nne, ikiwemo ya jana
ya fainali, ambapo Brazil iliibwaga Hispania kwa mabao 3-0. Kiungo wa Hispania,
Andres Iniesta, alipata tuzo ya Mpira wa Fedha, na mwenzake wa Brazil,
Paulinho, akashinda Mpira wa Shaba. Mshambuliaji wa Uhispania, Fernando Torres,
ameshinda Kiatu cha Dhahabu kwa kufunga mabao 5 katika michunao hiyo.
Mshambuliaji wa Brazil, Fred, alikuwa wa pili kwa kupata Kiatu cha Fedha, akiwa
pia na magoli 5, ingawa alicheza kwa dakika nyingi zaidi. Neymar alifunga
magoli 4 na kushinda Kiatu cha Shaba. Mlinda mlango wa Brazil, Julio Cesar,
alishinda Glavu ya Dhahabu, huku timu ya Uhispania ikipewa tuzo ya mchezo
mzuri.
0 comments:
Post a Comment