Mwanamke mmoja ameshitakiwa kwa madai ya kuiba chupi na fulana katika mtaa mmoja mjini Nakuru, Kenya.
Ilidaiwa kwamba Bi Teresia Muthoni aliiba chupi tatu na fulana moja katika mtaa wa Pangani Juni 24 mwaka huu. Mahakama iliambiwa kwamba aliiba vitu hivyo vya thamani ya KSh1,600 mali ya Bi Florence Wairimu.

Hata hivyo, mshukiwa alikanusha shtaka mbele ya Hakimu Mkuu Samuel Mungai na kuachiliwa kwa dhamana ya KSh30,000. Kesi hiyo itatajwa Julai 18 na itasikilizwa Agosti 26 mwaka huu.
Source: SwahiliHub
0 comments:
Post a Comment