Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
limepokea taarifa kwamba waandishi wa Habari kadhaa wamepelekwa Mtwara
kwenda kumhoji msichana mmoja kwa madai ya kubakwa na wananjeshi wa
JWTZ.
JWTZ linapenda kuwafahamisha
wananchi kuwa endapo taarifa hizo zitatangazwa kwenye baadhi ya vyombo
vya Habari wazipuuze kwani hazina ukweli wowote zaidi ya kuwa ni za
upotoshaji.
Msichana huyo amepandikizwa ili kuharibu taswira
nzuri ya JWTZ. Ifahamike kwamba maafisa na askari wa JWTZ waliopo huko
Mtwara wanafanya kazi kwa uangalizi wa karibu na vitendo hivyo vya aibu
hawawezi kuvifanya.
Jeshi letu linafanya kazi kwa nidhamu na si kama baadhi ya watu wenye maslahi binafsi wanavyolipaka matope.
Tunapenda kuwafahamisha watanzania wote kuwa JWTZ lipo kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote.
Tunasikitika
sana kama wapo watanzania wenye mawazo hayo machafu ya kulichafua JWTZ
lenye sifa nyingi ndani na nje ya nchi yetu.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 92023, Simu: 0764 742161
Monday, 1 July 2013
HOME »
» TAARIFA YA JWTZ YA KANUSHA KUHUSU TUHUMA UBAKAJI MTWARA
0 comments:
Post a Comment