Saturday, 6 July 2013

HATARI : DAWA ZA KICHINA ZA GUNDULIKA KUCHANGANYWA NA DAWA ZA KUULIA WADUDU

 
Dawa hizi zimekuwa zikitumika katika nchi mbalimbali kwa sasa

Licha ya kuaminiwa na kuchukuliwa kama tiba bora zaidi nchini, imegunduliwa kuwa dawa za mitishamba za Kichina zina chemchembe za dawa za kuulia wadudu.

Uchunguzi uliofanywa kupitia dawa hizo zilizonunuliwa katika maduka mbalimbali yanayouza dawa hizo nchini Uingereza umebaini kuwa dawa hizo zina kemikali zenye sumu zinazotokana na dawa za kuulia wadudu.

       Pamoja na  ukweli kuwa kemikali hizo zipo kwa kiasi kidogo sana , inasemekana matumizi ya dawa hizo kwa muda mrefu yanasababisha uharibifu katika Vichocheo, matatizo katika mfumo wa uzazi kwa wanaume na uharibifu wa mimba.
Zaidi ya Waingereza  milioni tatu hutumia dawa za Kichina kujitibu kwa maradhi mbalimbali kila mwaka.

'     Katika kipindi cha miezi sita kuanzia Novemba 2012 hadi  Aprili 2013,  wachunguzi wa Greenpeace walinunua aina saba tofauti za dawa za mitishamba zilizoingizwa kutoka China  kwa ajili ya kuzifanyia majaribio.
    
      Dawa hizo zilinunuliwa kutoka kwa wauzaji wa rejareja kutoka kwenye nchi saba tofauti ikiwamo Uingereza.
Dawa hizo ni miongoni mwa zile zinazoaminiwa zaidi na wauzaji hao na pia zinadaiwa kuwa tiba halisi ya magonjwa sugu ambayo yamekuwa wakiwasumbua watu wengi hususan katika jamii ya Waasia.
     
       Sampuli  26 kati ya  29 zilizochukuliwa kutoka Uingereza na maduka mengine barani Ulaya ziligundulika kuwa kuna chembechembe za dawa za kuulia wadudu.
Sampuli moja ya ‘honeysuckle’peke yake ilinunuliwa nchini Uingereza ilikuwa na viashiria 17 vya dawa hiyo ya kuulia wadudu, inayozidi nane katika kiwango cha usalama cha Ulaya

     Akitoa maoni yake kuhusiana na utafiti huo, mwanasayansi mkuu wa Taasisi Greenpeace ya Uingereza, Dk Doug Parr,  alisema‘Sumu zilizoko kwenye dawa hizi za kichina zinahatarisha afya za watumiaji wa dawa hizo”
  
      Watu wanaotumia dawa hizi kwa kuamini kuwa zinaponya haraka na kuboresha afya zao, washtuka sana kusikia kuwa dawa walizokuwa wakitumia kwa muda mrefu zina hatari na athari kubwa kwa afya zao. ‘Serikali ya Uingereza na Umoja wa Ulaya kwa ujumla wanatakiwa kuboresha mfumo wao wa uchunguzi wa usalama wa bidhaa kutoka China, ili kuwanusuru watumiaji wake.


Chanzo  mwananchi gazeti leo

0 comments: