Wednesday, 10 July 2013

TIMU MBILI ZA SOKA KUTOKA NIGERIA ZA FUNGIWA BAADA YA KUWEKA RECODI YA KUFUNGA BAO 79 -0 NA 67-0

Picture
 
Huenda Nigeria ikawa inadhihirisha ukweli kuhusu matokeo ya utafiti kuhusu vitendo vya rushwa kwani kwani taarifa kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari zinasema, timu nne za soka za nchini Nigeria zimefungiwa kwa muda na chama cha soka nchini humo huku zikisubiri kuchunguzwa kutokana na matokeo ya mechi zilizochezwa.

Timu hizo zilikutana katika mechi za mchujo ili kutafuta timu itakayopanda daraja, ila jambo la kushangaza ambalo limeingia katika vitabu vya kumbukumbu na historia ya mchezo huo, ni idadi ya magoli yaliyofungwa siku hiyo.

Zikicheza kwa wakati mmoja ila katika viwanja tofauti, timu moja Plateau United Feeders iliifunga nyingine, Akurba FC mabao 79-0 wakati timu ya Police Machine FC iliilaza nyenzake ya Bubayaro FC kwa mabao 67-0.

Matokeo ambayo ndiyo yaliyosababisha klabu zote zisimamishwe ili kupisha uchunguzi kubaini endapo rushwa na upangaji matokeo vilifanyika, jambo ambalo Wanigeria wengi wanaamini ndivyo lilivyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa nchini humo ambavyo vimeingilia soka kiasi cha kusababisha watu wakose hamu ya kutizama mechi na kufuatilia ligi hiyo kwa kuamini kuwa tayari zimeshapangiwa matokeo, badala yake wananchi wameamua kutizama na kufuatilia vilabu na ligi za Uingereza na Uhispania.

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya nchi hiyo aliwahi kujiuzulu kwa kusema ameshindwa kuchukuliana na vitendo vya rushwa vilivyokithiri katika soka nchini humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji ya Nigerian Football Federation (NFF), Muke Umeh alisema matokeo ya mechi hizo hayakubaliki na ni kashfa kubwa.

Amesema adhabu kubwa itatolewa ikiwa uchunguzi utabaini makosa yanayosadikiwa kufanywa kwa makusudi.

Timu zote zilikuwa zikiwania kupanda daraja la ligi lakini kila mmoja ilihitaji kuipiku nyingine kwa wingi wa magoli ambapo matokeo hayo yaliyobatilishwa, yalikuwa yameifanya Plateau United Feeders iipiku Police Machi

0 comments: