Mzee afumaniwa akichinja mbwa nchini kenya
MZEE mwenye umri wa miaka sabini
anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kimilili akisubiri kufikishwa
mahakamani, baada ya kufumaniwa na wananchi akichinja mbwa.
Akithibitisha
kisa hicho kinara wa polisi wa Kimilili Philip Wambugu alisema kuwa
Samwel Ng’ang’a alifumaniwa nyumbani kwake akimchinja mbwa wake ambaye
amekuwa akimfuga kwa muda wa miezi mitatu.
Hii ni baada
ya polisi kupashwa habari kutoka kwa mmoja wa majirani wa mzee huyo,
ambaye hakutaka jina lake litajwe, ya kuwa mzee huyo alikuwa amejifungia
ndani ya chumba chake akimtoa ngozi mbwa huyo.
Wambugu
aliongeza kuwa mzee huyo atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kutathmini
hali yake ya kiakili kabla ya kufikishwa mahakamani.
Juhudi za KNA
za kutaka kujua ni nini hasa kilichomfanya mzee huyo kufanya kitendo
hicho zilifichua kuwa mzee huyo anaugua ugonjwa wa kifafa jambo ambalo
anasema kuwa alipania kulifanya baada ya kumtembelea mganga akitafuta
suluhu ya ugonjwa huo na hivyo anafuata maagizo ya mganga huyo.
Naye afisa
mkuu wa wanyama katika eneo hilo, Joseph Ganda alisema kuwa mbwa hayupo
kati ya orodha ya wanyama wanaoliwa na binadamu na ni hatia kwa mzee
huyo kutekeleza kitendo hicho.
Mzee huyo sasa atashtakiwa kulingana na sheria za wanyama.
chanzo swahilihub.com
0 comments:
Post a Comment