Uamuzi dhidi
ya kesi inayowakabili wanachama watano wa Chadema yaliyokuwa yatolewe
jana sasa yatatolewa Agosti 5. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Tabora, Simon Lukelelwa alitoa uamuzi huo kufuatia kuchelewa kufika kwa
washtakiwa wa kesi hiyo waliohifadhiwa Gereza la Uyui Tabora.
Wakati
uamuzi huo ukitolewa na Jaji Lukelelwa, washtakiwa wote watano wa kesi
hiyo, Henry John Kileo, Evodius Justian, Oscar Kaijage, Seif Kabuta na
Rajab Kihawa hawakuwa katika chumba cha mahakama muda wa saa tatu na
nusu asubuhi.
Washtakiwa
walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa nne na dakika arobaini na
waliarifiwa na wakili mwakilishi, Emanuel Msyani kuwa shauri limepangwa
tarehe tano mwezi ujao wakiwa ndani ya chumba cha mahabusu ya Mahakama
Kuu.
Wakili
Msyami alisema Mahakama Kuu iliridhia ombi la upande wa Jamhuri kuomba
kuongezewa muda angalau kwa siku moja kwa vile walipokea hoja Ijumaa
iliyopita.
Aliongeza
kuwa Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na kuongeza muda hadi tarehe moja
uwe umewasilisha majibu ya hoja na kuipanga tarehe tano kwa ajili ya
uamuzi.
Kesi hiyo ya
rufaa ya jinai namba 53/2012 ilifunguliwa na Wakili wa Utetezi, Peter
Kibatala na kuanza kusikilizwa Julai 22 mwaka huu mbele ya Jaji
Lukelelwa ikiomba miongozo ya kisheria ikiwemo yaliyotolewa na mahakama
za wilaya na mkoa.
Shauri la
maombi ya marejeo liliwakilishwa na Wakili Peter Kibatala anayewatetea
washitakiwa, akiiomba mahakama kuu ipitie majalada ya kesi mbili dhidi
ya wateja wake zilizofunguliwa mahakama hizo baada ya kuona maamuzi yake
hayakutenda haki.
Wakili
Kibatala alibainisha katika maombi hayo kwamba kutokana na maamuzi hayo
ya mahakama za chini yameathiri pia haki za waomba rufaa ikiwa ni pamoja
na kuwanyima haki ya kupata dhamana.
Kwa upande
wake Serikali ilishindwa kujibu maombi hayo, badala yake ilijenga hoja
kwamba walichelewa kupata nyaraka hizo kwani walizipokea siku moja kabla
ya kutajwa shauri hilo hivyo walishinda kuzijibu.
0 comments:
Post a Comment