Sunday, 14 July 2013

TANZANIA IMEWAPOTEZA WANAJESHI SABA (7) DARFUR NCHINI SUDANI

Tanzania imewapoteza wanajeshi wake saba saba kuyokana na shambulizi la kushitukiza liliyofanywa na waasi wanaopigana na Serikali ya Sudan ambao pia waliharibu vifaa vya wanajeshi hao na kuwaacha wanajeshi 17 majeruhi (wawili kati yao ni wanawake).

Wanajeshi hao walikuwa ni sehemu ya  kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha kulinda amani katika jimbo hilom

Miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri taratibu za kusafirishwa kwa maziko nyumbani Tanzania.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Kimoon amelaani mauaji hayo na kusema anatarajia Serikali ya Sudan itachukua hatua madhubuti kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei ena.

Hii ni mara ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.

Agosti mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye tukio kama hilo.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe alipoulizwa na gazeti la MWANANCHI kwa njia ya simu  kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.

Tanzania imechangia jeshi la askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la Darfur.

0 comments: