LHRC: Tutamshtaki Waziri Mkuu mahakamani
kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”
Alijibu: “Ni lilelile nililosema... Mwishowe
unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa
usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... Hamna namna nyingine,
maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya
kisheria. “Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara
zaidi... Wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige
tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... Maana tumechoka.”
Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana wakati akitoa ripoti ya utafiti ya miezi sita kuhusu mambo mbalimbali ya haki za binadamu kuwa kituo hicho kiko katika hatua za mwisho za kupeleka shauri hilo Mahakama Kuu ili kumfungulia kesi Waziri Mkuu.
“Kauli ya Pinda inavunja Katiba ya nchi ya usawa
mbele ya sheria ambayo ni Ibara ya 13 (1). Hivyo tumekusudia kumfungulia
kesi Waziri Mkuu ambaye amevunja Katiba,” alisema.
Sungusia alisema kauli hiyo iliyotolewa na
kiongozi wa juu wa Serikali ni kinyume cha Katiba, sheria za nchi na
misingi ya haki za binadamu hivyo.
“Pinda alitoa kauli ile kama msimamo wa Serikali, tulitarajia angefuta kauli yake aliyotoa bungeni ya kuwabariki polisi kupiga raia katika mkutano ulioisha wa Bunge la Bajeti lakini hakufanya hivyo,” alisema.
Ofisi ya Waziri Mkuu wajibu
Akizungumza madai hayo jana, Katibu wa Waziri
Mkuu, Deusdedit Buberwa alisema: “Hayo unayoniambia ni mapya kabisa.
Mimi sifahamu chochote, kwani sijaona hata barua yao. Ningeweza
kuzungumza kama ningepata barua au hata kusikia, lakini hakuna hicho
kitu.”
Utafiti wa mauaji
Akitoa taarifa ya utafiti huo, Mtafiti wa LHRC, Pasience Mloe alisema katika kipindi cha miezi sita mwaka huu, kumekuwa na vifo 303 vilivyotokana na imani za kishirikina.
Alisema idadi hiyo ni kubwa kwani inakaribia sawa
na takwimu za mwaka mzima wa 2012 ambao watu 336 walipoteza maisha kwa
sababu hizohizo.
Mloe alisema utafiti huo ulibaini kuongeza kwa
ubakaji wa watoto kwani katika kipindi hicho cha miezi sita, 394
walifanyiwa ukatili huo.
0 comments:
Post a Comment