Hali ya kiafya ya shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela imeendelea kuwa tata na inasemekana kuwa ndugu na jamaa wa mwanasiasa huyo mkongwe hawana matumaini tena na kupona kwake.
Mwana wa kike wa Nelson Mandela, Makaziwe Mandela, amewaambia waandishi habari mjini Pretoria kwamba hali ya baba yake ni mbaya na kwamba kila kitu kinaweza kutokea. "Hali ya baba ni mbaya sana na kila kitu kinaweza kutokea, ingawa Mwenyezi Mungu ndiye anayejua wakati wa kuondoka", amesisitiza Makaziwe.
Hali mbaya ya kiafya ya Mzee Nelson Mandela imemlazimisha Rais Jacob Zuma kuvunja safari yake nje ya nchi. Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Zuma kusitisha shughuli zake za umma tangu Mandela alazwe hospitalini mapema mwezi huu.
Wakati huo huo idadi kubwa ya watu imeendelea kukusanyika mbele ya hospitali ya matibabu ya moyo mjini Pretoria wakimuombea dua shujaa wa nchi yao.
0 comments:
Post a Comment