Taarifa za kituo kimoja cha habari zinasema kuwa mchambuzi wa masuala ya
kijeshi wa utawala wa Israel, Rooney Daniel amefichua kuwa Waziri wa
Ulinzi wa Misri, Abdul Fatah Al-Sisi, aliitaarifu Israel kuhusu kuwepo
kwa njama za kumpindua Rais Muhammad Morsi wa nchi hiyo siku tatu kabla
ya tukio hilo.
Taarifa hizo zinasema kuwa Rooney Daniel
akizungumza kupitia chaneli ya televisheni ya utawala huo, amesema kuwa
Al-Sisi aliutaka utawala wa Israel kuimarisha ulinzi dhidi ya Harakati
ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, HAMAS, kwa kuhofia kuwa inaweza
kutoa radiamali kali dhidi ya Misri.
Aidha amesema kuwa, Al-Sisi
aliwambia viongozi wa Tel Aviv kwamba, anaiogopa harakati ya HAMAS na
Israel ilimuhakikishia waziri huyo wa ulinzi wa Misri kwamba, itaweka
ulinzi mkali katika mipaka ya Ukanda wa Ghaza ili kuzuia hatua zozote
zinazoweza kuchukuliwa na HAMAS.
Kwa upande wake utawala wa
Israel ulimtaka Al-Sisi kuharibu njia za chini kwa chini zinazotumiwa na
wakazi wa Ukanda wa Ghaza mkabala na ulinzi huo wa Israel.
Wednesday, 24 July 2013
HOME »
» MISRI YA ILITAARIFU ISLAEL KABLA YA KUMPINDUA MORSI
0 comments:
Post a Comment