POLISI Mkoa wa Kusini Pemba, limewataka
wananchi kuwa na utamaduni wa kuvumiliana kidini na kuheshimu imani za
wengine, kwa kuepuka kula hadharani katika mfungo wa mwezi mtukufu wa
Ramadhani kwani kufanya hivyo kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani
miongoni mwa jamii.
Jeshi hilo limesema limejipanga
kukabiliana na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani kama vile uvaaji
wa mavazi yasioendana na maadili ya kiislamu na kuhakikisha
linakabiliana na uhalifu na wahalifu.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Saleh
Mohammed Saleh, alitoa onyo hilo wakati akizungumza na mwandishi wa
habari hizo ofisini kwake Madungu -Chake Chake Pemba.
“Tumejipanga vyema kufanya doria na
oparesheni mbali mbali za kuwasaka wahalifu wote ili kuona wananchi wa
mkoa wa Kusini wanatekeleza ibada yao kwa salama na amani,” alisema.
Na Maryam Salim, Pemba
0 comments:
Post a Comment