BAADHI ya abiria wanaosafiri kwenda na kuingia jijini Dar es
Salaam wanatarajia kukumbwa na adha ya usafiri leo kwa muda wa saa
kadhaa wakati Rais wa Marekani, Barack Obama, atakapotembelea mitambo
ya kuzalisha umeme ya Symbion Power iliyopo eneo la Ubungo.
Akizungumza na gazeti laTanzania daima jana, Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, Mohammed Mpinga, alisema kuwa kituo kikuu cha mabasi
yaendayo mikoani cha Ubungo (UBT), kitafungwa kuazia saa 3:00 asubuhi
hadi saa 7:00 mchana.
Alisema kituo hicho kitasitisha safari zake
kutokana na kufungwa kwa Barabara ya Morogoro ambako kipo kituo hicho
.“Kituo hicho kinafungwa ili kupisha msafara wa rais huyo wakati
atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Symbion Power,”
alisema Mpinga bila kufafanua kama kutakuwa na njia mbadala.
Licha ya kufungwa kwa muda kituo hicho vilevile mabasi yanayotoka
mikoani yatazuiwa kuingia mjini hadi saa 7:00 mchana wakati rais huyo
atakapokuwa amemaliza ziara yake kwenye mitambo hiyo.
Mpinga aliongeza kuwa mbali na UBT, pia kituo kidogo cha daladala na
magari ya shamba kitafungwa kuanzia asubuhi hadi baada ya kumalizika kwa
ziara hiyo, ambapo madereva wote wanatakiwa kutafuta njia nyingine za
ndani ili kuepuka usumbufu kwa abiria.
Kamanda huyo aliwaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu utakaojitokeza kutokana na kufungwa kwa barabara hizo.
chanzo na Shehe Semtawa Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment