Mtandao
wa magazeti ya GPL umechapisha habari ya kumnasa msichana, Furaha (16),
aliyekomea elimu ya msingi, darasa la saba, akiuza dawa katika duka la
madawa ya binadamu.
GPL inasema ililazimika kuchunguza na kuandika habari hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali wakidai mhusika, Mama Atu, wa pharmacy hiyo iliyopo Goroka, Toangoma huko Kongowe wilayani Temeke mkoani Dar es Salaam, humwachia Furaha auze dawa kwa kubahatisha na mara kadhaa wagonjwa hupewa dozi ndivyo sivyo huku yeye akiwa anajishughulisha na kazi nje ya pharmacy.
“Kuna mwenzetu alikuwa akiugua ugonjwa mwingine, alipofika pale aliandikiwa dawa za malaria, hali yake

ikawa mbaya
hadi akakimbizwa hospitalini kulazwa, tulipomuonya mmiliki hakutusikia,”
alisema mmoja wa watu wanaoijua suala hilo kwa undani.
Ili kupata ushahidi kamili, mwanahabari wa GPL alijifanya mgonjwa na kwenda kwenye pharmacy hiyo kuomba ushauri wa matibabu.
Baada ya kumsikiliza, Furaha alimtajia dawa za ugonjwa wa typhoid lakini mwanahabari huyo alimkwepesha na kumuomba dawa aina ya chloroquine ambapo Furaha alikubali na kutaka kumpa.
Baada ya kushuhudia hayo GPL ilimfuata mwenyekiti wa mtaa huo, Issa Shomari kupitia mjumbe wake na kufika katika pharmacy hiyo kujionea hali halisi ambapo kama ilivyokuwa mwanzo hausigeli huyo alikuwa tayari kutoa huduma.
Baada ya kikosi kazi kujitambulisha na kumhoji, alikiri kuwa yeye ni mtumishi wa ndani, ana miaka 16, elimu ya darasa la saba, mwenyeji wa Iringa, na huwa anaachiwa auze na mwajiri wake na hutoa dawa za malaria na magonjwa anayoyafahamu.
Akizungumza kwa mshtuko baada ya kujionea hali halisi, mwenyekiti huyo wa mtaa alisema kuwa atahakikisha anawasiliana na Kamati ya afya ya Wilaya ya Temeke ili kuyafuta maduka kama hayo mtaani kwake.

0 comments:
Post a Comment