Tuesday, 2 July 2013

MWANAFUNZI (15)AMBAYE ANASADIKIWA KIBAKA ANUSURIKA KUAWAWA

KIBAKA Rajabu Hamisi Juma (15), Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Msasani, iliyoko Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, amenusurika kuuwawa na wananchi wenye Hasira kali baada ya kufamaniwa mchana wa leo akiiba katika Duka la mfanyabiashara Paulo Maile.

Kibaka huyo ambaye ni mkazi wa Pasua, amekutwa na masahibu hayo baada ya kuingia dukani hapo kwa kudhani kuwa mhudumu wa duka yuko mbali na ndipo alipokutwa akiwa tayari ameshaiba Simu, aina ya Nokia huku akijaribu kuficha Laptop iliyokuwa dukani hapo.

Akizungumzia mkasa huo, kibaka Rajabu huyo aliamua kufanya hivyo kwa ajili ya kukosa ada ya kulipa shule kutokana na wazai wake kukataa kumlipia ada anayodaiwa shuleni hapo.



Tukio hilo lililowaacha mdomo wazi baadhi ya mashuhuda waliofika dukani hapo , limetokea leo majira ya saa 6:10 mchana katika duka la Nguo lililloko katika mtaa wa double Road, barabara kuu ya Moshi-Dar es salaam linalomilikiwa na mfanyabiashara Paulo Maile mkazi wa Soweto.


Kamera ya .MTANDAO HUU  ilifika katika eneo la tukio na kukuta kijana huyo akishushiwa kipondo na mhudumu wa duka hilo aliyefahamika kwa jina moja la George.Huu hapa ni mkanda mzima wa tukio lenyewe:
Amando Tarimo ambaye ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo akishusha kipondo kwa kijana Rajabu Hamisi aliyekutwa akijaribu kuiba katika duka la mfanyabiashara Paulo Maile, Leo Mchana.



Gari la Polisi likiondoka na mhalifu katika eneo la tukio


Vijana wa Boaz wakiondoka na Kibaka huyo aliyenusirika kufa mikononi mwa Raia Wema


George akitoa Maelezo kwa mashuhuda wa tukio la wizi nje ya duka hilo


George aendelea na Maelezo


Kibaka  Rajabu Hamisi (Jezi ya Manchester Utd) akiomba msamaha baada ya kufumaniwa dukani katika jaribio la wizi, Paulo Maile ambaye ndiye mmiliki wa Duka (shati la mistari), George (shati jekundu katikati) na mmoja wa mashuhuda wakimsikiliza kibaka huyo dukani hapo


Rajabu akipakizwa kwenye gari la polisi leo mchana


Mwenye duka akitoa kipondo kwa Kibaka huyo...


kipondo kikiendelea...


 

Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo, Amando Tarimo akiendeleza kipondo kwa kibaka huyo....

   

0 comments: