CHELSEA YAILAZA ‘MTU 10’ SPURS 4-0!
ETO’O ASHEREHEKEA BAO KAMA ‘KIZEE’, KEJELI KWA MOURINHO!
LIGI KUU ENGLAND
MATOKEO:
Jumamosi Machi 8
West Brom 0 Man United 3
Cardiff 3 Fulham 1
Crystal Palace 0 Southampton 1
Norwich 1 Stoke 1
Chelsea 4 Tottenham 0
CHELSEA wamejichimbia kileleni mwa Ligi Kuu England kwa kuichapa Tottenham Bao 4-0 na kuongoza Ligi wakiwa Pointi 7 mbele.
Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0.
Kipindi cha Pili, makosa ya Jan
Vertonghen yaliwafungulia Chelsea mvua ya Magoli baada ya kuteleza akiwa
na Mpira na katika jitihada za kuokoa akatoa pasi kwa Samuel Eto’o
ambae alifunga na kusherehekea kama Mtu Mzee ikiwa ni ishara ya
kumkejeli Meneja wake Jose Mourinho ambae Wiki iliyopita alirekodiwa
akisema hajui Umri wa Eto’o na hilo kuibua utata kuhusu Umri wa Straika
huyo toka Cameroun.
Bao hilo lilidumu Dakika 5 tu na kwenye
Dkika ya 60 Tottenham walipata mapigo mawili baada Refa Michael Oliver
kuwapa Penati Chelsea na pia kumpa Kadi Nyekundu Sentahafu wao Younes
Kaboul kwa kumchezea Rafu Samuel Eto’o.
Eden Hazard alifunga Penati hiyo na Chelsea kuongoza 2-0.
Chelsea waliongeza Bao nyingine, zote
kupitia Demba Ba alieingizwa badala ya Eto’o katika Dakika ya 76, na
zote zilitokana na makosa ya Mabeki wa Tottenham huku moja likifungwa
baada Sandro kuteleza na jingine Kichwa cha Kyle Walker kunaswa kabla
kumfikia Kipa Hugo Lloris.
VIKOSI:
CHELSEA: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Lampard, Matic, Ramires, Hazard, Schurrle, Torres
Akiba: Oscar, Mikel, Ba, Willian, Schwarzer, Eto'o, Kalas.
TOTTENHAM: Lloris, Naughton, Dawson, Kaboul, Vertonghen, Sandro, Bentaleb, Walker, Sigurdsson, Lennon, Adebayor
Akiba: Paulinho, Soldado, Townsend, Chadli, Friedel, Fryers, Kane.
Refa: Michael Oliver
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Chelsea |
29 |
34 |
66 |
2 |
Liverpool |
28 |
38 |
59 |
3 |
Arsenal |
28 |
24 |
59 |
4 |
Man City |
26 |
42 |
57 |
5 |
Tottenham |
29 |
0 |
53 |
6 |
Man United |
28 |
12 |
48 |
7 |
Everton |
27 |
11 |
48 |
8 |
Newcastle |
28 |
-2 |
43 |
9 |
Southampton |
30 |
2 |
42 |
10 |
West Ham |
28 |
-4 |
31 |
11 |
Aston Villa |
28 |
-7 |
31 |
12 |
Stoke |
29 |
-14 |
31 |
13 |
Hull |
28 |
-5 |
30 |
14 |
Swansea |
28 |
-4 |
29 |
15 |
Norwich |
29 |
-22 |
29 |
16 |
Crystal Palace |
28 |
-19 |
27 |
17 |
West Brom |
28 |
-11 |
25 |
19 |
Cardiff |
29 |
-28 |
25 |
18 |
Sunderland |
26 |
-16 |
24 |
20 |
Fulham |
29 |
-36 |
21 |
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Machi 15
1545 Hull v Man City
1800 Everton v Cardiff
1800 Fulham v Newcastle
1800 Southampton v Norwich
1800 Stoke v West Ham
1800 Sunderland v Crystal Palace
1800 Swansea v West Brom
2030 Aston Villa v Chelsea
Jumapili Machi 16
1630 Man United v Liverpool
1900 Tottenham v Arsenal
0 comments:
Post a Comment